Ripoti
ya itv.co.tz imeamplfy kwamba mwanamke mmoja raia wa Nigeria amekamatwa
na maofisa usalama wa mamlaka ya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar-es-salaam akiwa na kete 99 za dawa za kulevya
alizokuwa amezihifadhi kwenye chupa ya mafuta ya kupaka na nyingine
kwenye kopo la poda za watoto, akijianda kusafiri nazo hadi Rome Italia
kupitia ufaransa.
Meneja
mkuu wa usalama wa uwanja wa ndege Clemence Jungu amesema kukakamtwa
kwa dawa hizo kunafuatia uwanja huo kufungwa mashine za kisasa za
kukagulia mizigo ikiwemo dawa za kulevya.
Kwenye
sentensi nyingine, raia mmoja wa Urusi aitwae Romani Demichenco
akitokea Berlin Ujerumani kupitia Doha Qatar amekamatwa kwenye uwanja wa
ndege Dar es salaam akiwa na vivimiminika vinavyoweza kusababisha
milipuko ambapo tayari amefikishwa Mahakamani.
No comments:
Post a Comment