Tuesday, February 9, 2016

ALICHO KISEMA ADAM JUMA KUUSU VIDEO MPYA YA ALIKIBA "LUPELA".


ENTERTAINMENTDirector Adam Juma ameyaandika haya baada ya kuitazama video mpya ya Alikiba ‘Lupela’

Siku moja baada ya staa wa bongofleva Alikibakuiachia video ya ngoma yake ‘Lupela‘, leo Director wa long time Tanzania Adam Jumaameyatoa yake ya moyoni kupitia account yake ya instagram baada ya kuona comments za watu wengine wakiikosa video yenyewe.

“Lupela @officialalikiba , this is art, watanzania hatujui kuidadavua art. Hatujui thamani ya kitu, tunachukulia kiurahisi urahisi tu, kila mtu anajifanya anajua kitu ambacho sio sawa. Hii sio video tu, tulia basi angalia kwa umakini utapata ujumbe usipoelewa inawekana tatizo lipo kwenye level yako ya kuchanganua ujumbe ktk picha, btw sio fan wa alikiba ni mwana tu. Ningependa kusema video ni A one, haifanani na kitu ambacho tumezoe!!! Go kiba…...” – Adam Juma

JOH MAKINI AWEKA HISTORIA IRINGA.

Ni Joh Makini kwenye stage Iringa Tanzania…. anasema hii ni moja ya show alizowahi kufanya ndani ya January (mwezi dume) na zikauza ticket mpaka Promota akaamua kuongeza kiingilio baada ya kuona watu wanazidi kuingia.
Mashabiki walifurika sehemu ya show kiasi ambacho ata promota akutarajia kama watu wangejaa kiasi hicho.

Sunday, January 10, 2016

Mbwana samata akabidhiwa unahodha wa Timu ya Taifa.

Mara baada ya mchezaji mbwana samata kutwaa  Tunzo ya mchezaji bora wa Afrika kati ya wale wachezajo wa ndani,Kocha mkuu wa timu ya Taifa chars boni mkwasa ameamua kumtunuku mbwana samata unahodha wa timu ya Taifa.kocha huyo alinukuliwa kwa maneno haya "Ni mabadiliko ya kawaida hasa baada ya Mbwana kutwaa tuzo na heshima kubwa kwa Afrika, sisi tumeona tumuongezee majukumu mengine ili aweze kutuongozea timu yetu ya taifa Taifa Stars, ameweza kuiongoza TP Mazembe kuwa Bingwa wa Afrika, hivyo tumeona tumpe fursa hii ili awaongoze wenzake katika mechi za AFCON zilizobaki".

Sunday, August 31, 2014

KUHUSU GARI LA IKULU YA KENYA LILILO IBIWA

Screen Shot 2014-08-30 at 1.45.28 PM 
Ni moja kati ya zile stori za nadra sana kuzisikia yani, kwa uoga au ulinzi mkali ambao huwa unawekwa kwenye vitu vya serikali tena sehemu kama Ikulu ni nadra sana kusikia kuna jamaa wamejihami na kuiba.
Labda inawezekana hawa jamaa hawakuwa wanajua kama ni gari la Ikulu, aliekua analiendesha ni Askari akielekea kwenye makazi ya Askari lakini ghafla barabarani Nairobi akavamiwa na watu watatu waliokua na silaha aina ya AK 47.
Ilikua saa mbili usiku ambapo walimshusha wakamvua nguo na kumtupa kwenye mtaro alafu wakaondoka na gari ambalo ni miongoni mwa magari machache ya Ikulu yasiyopenya risasi.
Ni gari aina ya BMW ambalo huwa linakuwepo kwenye msafara wa Rais Uhuru Kenyatta ambapo kweli Ikulu imethibitisha gari hilo kuwa lake na kwamba msako wa kulitafuta na waliohusika pia unaendelea. – Manoa Esipisu msemaji wa Ikulu.

Saturday, August 16, 2014

UKWELI KUHUSU TETESI ZA UGONJWA WA EBOLA KUINGIA TANZANIA.

Screen Shot 2014-08-15 at 10.47.21 AMUgonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umeingia kwenye headlines za dunia kutokana na kuripotiwa kwenye nchi mbalimbali za Afrika sasa umeingia kugusa vichwa vya habari na kuihusisha Tanzania.
Waziri wa Afya wa Seif Rashid amesema wagonjwa waliohisiwa kupata maambukizo hayo kutokana na dalili za awali ni kutoka Benin na Mtanzania lakini baada ya vipimo wameonekana hawana maambukizo hayo.

 

Ugonjwa wa Ebola ambao kwa sasa umeingia kwenye headlines za dunia kutokana na kuripotiwa kwenye nchi mbalimbali za Afrika sasa umeingia kugusa vichwa vya habari na kuihusisha Tanzania.
Waziri wa Afya wa Seif Rashid amesema wagonjwa waliohisiwa kupata maambukizo hayo kutokana na dalili za awali ni kutoka Benin na Mtanzania lakini baada ya vipimo wameonekana hawana maambukizo hayo.
Screen Shot 2014-08-15 at 10.47.06 AMWaziri Seif Rashid amesema kuwa tayari eneo maalumu limetengwa kwa ajili ya kufanyia uchunguzi wagonjwa wanaotiliwa shaka kuwa na ugonjwa huo ikiwa ni kauli iliyotoka baada ya kufanyiwa uchunguzi kwa wagonjwa wawili waliohisiwa.
Kupitia ukurasa wake wa facebook, Waziri Seif amesema vifaa maalumu vitakavyotumiwa na watoa huduma katika kuhudumia wagonjwa vimewekwa pia huku wizara ya afya ikiongeza uwezo wa kufanya uchunguzi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere ambao wasafiri wengi kutoka nje huutumia